Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
MKURUGENZI MTENDAJI WRRB AFANYA KIPINDI MAALUM CLOUDS TV KUELEKEA KIKAO CHA MAMENEJA DHAMANA
20 Jan, 2026
MKURUGENZI MTENDAJI WRRB AFANYA KIPINDI MAALUM CLOUDS TV KUELEKEA KIKAO CHA MAMENEJA DHAMANA

MKURUGENZI MTENDAJI WRRB AFANYA KIPINDI MAALUM CLOUDS TV KUELEKEA KIKAO CHA MAMENEJA DHAMANA

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala , Bw. Asangye Bangu leo 19 Januari 2026 amefanya mahojiano mubashara katika kipindi maalum cha Clouds 360 akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa kampuni ya Meneja Dhamana(CGS Collateral Co.ltd Bw.Cliff Shedrack, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kwenye mkutano wa wadau wa mfumo na meneja dhamna nchini.

Kikao hicho kinachotarajiwa kufanyika januari 20 2026 jijini Dar es salaam kitacho kutanisha wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za fedha,kampuni za meneja dhamana,wafanya biashara na wawakilishi wa wakulima ambapo hoja muhimu kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi, usimamizi wa mazao na maendeleo ya mfumo wa stakabadhi za ghala zitajadiliwa kwa kina.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi mtendaji ametoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake mahiri na kwa kuendelea kuiwezesha WRRB kutekeleza majukumu yake ki ufanisi kwa manufaa ya wakulima na Taifa kwa ujumla.

Bw. Bangu amesema kuwa mageuzi makubwa yaliyofanywa na Serikali katika sekta ya    kilimo na biashara yameleta matokeo chanya, hususani katika kuimarisha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, kuongeza uaminifu kwa wadau, na kuchochea ukuaji wa soko la mazao nchini. 

"Ushirikiano huu umeleta tija kubwa katika kuongeza thamani ya mazao na kuinua kipato cha wakulima,” alisema Bwa Bangu