Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
Dira na Dhamira

Dhima

Kuwa msimamizi wa ghala kimataifa.

Dhamira

Kuchochea maendeleo ya uchumi wa bidhaa na wamiliki wa ghala kwa kusimamia ghala na kuhakikisha usawa na upatikanaji endelevu wa huduma za fedha, mifumo ya masoko ya mazao na bei ya ushindani.

Maadili ya Msingi

  1. UADILIFU - tunahakikisha kuwa mikataba yote na shughuli zote zinafanywa kwa umahiri wa hali ya juu, ubora na weledi.
  2. UWAJIBIKAJI- tunahakikisha maamuzi yanayotekelezeka kupitia sheria zinazotabirika na pia ushiriki kamili wa wadau wa mfumo wa stakabadhi ghalani.
  3. TUNAJALI WATU - sisi ni mwajiri anayejali ambaye kupitia kazi ya timu zetu, huwahudumia wadau wa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa uweledi wa hali ya juu na wa kutosha
  4. UWAZI - tunatimiza agizo letu kwa njia ya kimaadili na wazi kwa kuheshimu sheria na utumiaji sahihi wa taarifa rasmi.
  5. HESHIMA -tunaheshimiana,tunaheshimu wateja wetu, bila upendeleo katika huduma na heshima kwa wote.
  6. UTAWALA BORA - Sisi ni viongozi wa kushughulikia maswala ya rushwa, kutazama haki na uamuzi wa wakati unaofaa
  7. UAMINIFU KWA SERIKALI - tunatii maagizo ya serikali.