Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
WRRB IMEKUTANA NA WADAU MUHIMU WA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA TAREHE 20 JANUARI 2026 KUJADILI UTEKELEZAJI WA MFUMO WA MENEJA DHAMANA NCHINI.
22 Jan, 2026
WRRB IMEKUTANA NA WADAU MUHIMU WA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA TAREHE 20 JANUARI 2026 KUJADILI UTEKELEZAJI WA MFUMO WA MENEJA DHAMANA NCHINI.

WRRB imekutana na wadau muhimu wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala tarehe 20 Januari 2026 kujadili utekelezaji wa Mfumo wa Meneja Dhamana nchini.

Mkutano huo uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, ukijumuisha Taasisi za Fedha, Mameneja Dhamana, Waendesha Ghala, Wafanyabiashara na Taasisi za Umma.

Dkt. Serera alisisitiza kuwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ni mkombozi kwa wananchi na wafanyabiashara, na unahitaji ushirikiano wa Serikali, Taasisi za Kifedha na Sekta Binafsi ili kuleta tija kwa biashara, viwanda na masoko ya taifa.