Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
WRRB YAWAFIKIA WADAU ‘MAZAO CONNECT’
15 Sep, 2026
WRRB YAWAFIKIA WADAU ‘MAZAO CONNECT’

BODI ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imetoa elimu kuhusu Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa wadau wa sekta ya kilimo kupitia kikao kilichoandaliwa na Mazao Connect.

Afisa Ubora wa WRRB, Bw. Antolious Kabyemela, akizungumza katika kikao hicho mwishoni mwa wiki, ameeleza namna mfumo huo unavyowaunganisha wakulima, waendesha ghala, wanunuzi na taasisi za fedha katika mnyororo wa biashara ya bidhaa.

Pia, amefafanua taratibu za upokeaji wa bidhaa ghalani na umuhimu wa kuzingatia ubora katika uhifadhi na biashara ya bidhaa, hatua inayosaidia kuongeza thamani na ushindani wake katika soko.

Amesema Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unarahisisha ukusanyaji wa pamoja wa bidhaa, udhibiti wa ubora, kuongeza thamani, kuwapa wazalishaji nguvu katika soko na kuwaunganisha na masoko ya ndani na nje ya nchi. 

Aidha, mfumo huo unachangia kuongeza fursa za ajira, hususan katika maeneo ya vijijini.

Mazao Connect inawakutanisha wadau mbalimbali, wakiwamo wakulima na wafanyabiashara, kwa lengo la kuunganisha fursa na kuimarisha biashara ya mazao.

 

slot gacor