Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
BODI YA USIMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA (WRRB) NA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO
07 Oct, 2025

Dodoma, Oktoba 7, 2025 — Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo wametiliana saini makubaliano ya ushirikiano (MoU) yanayolenga kuimarisha matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika sekta mbalimbali 

Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu, na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Kupitia makubaliano hayo, pande hizo mbili zitashirikiana katika tafiti za pamoja na ubunifu wa mfumo ya kidijitali kwa ajili ya matumizi katika ghala , ili kuboresha ufanisi na uwazi katika mfumo ya stakabadhi za ghala nchini.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Bangu, amesema kuwa kupitia ushirikiano huo, wanafunzi wa UDOM watapewa fursa za kufanya mafunzo kwa vitendo (field work) ndani ya miradi hiyo ya kidijitali. Hatua hiyo inalenga kuwajengea uwezo na uzoefu wa kazi vijana wanaomaliza chuo, ili waweze kuwa sehemu ya suluhisho katika kukuza teknolojia na ubunifu nchini.

Kwa upande wake, Prof. Kusiluka amepongeza ushirikiano huo akisema utakuwa kichocheo muhimu katika kukuza tafiti zenye tija na kutengeneza mifumo ya kiteknolojia inayoweza kutumika katika sekta mbalimbali za uchumi.