MKUTANO WA WADAU WA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA GEITA
MKUTANO WA WADAU WA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA GEITA
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mheshimiwa Martine Shigela, Leo tarehe 18.12.2025 amefungua rasmi na kushiriki Mkutano wa Wadau wa mazao ya Choroko, Dengu na Alizeti. Katika mkutano huo, Mheshimiwa Shigela amesisitiza umuhimu wa kutumia mifumo sahihi na rasmi ili kuimarisha uzalishaji na masoko ya mazao. Aidha, ameelekeza viongozi wa Wilaya na Halmashauri kuhakikisha elimu ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala inawafikia wakulima kabla ya kuanza kwa msimu wa mauzo ya Choroko. Watalam wa kilimo kuendelea na zoezi la upimaji wa udongo na kushauri wakulima kanuni bora za kilimo ili kuongza tija.
Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waheshimiwa Wabunge, Wakuu wa Idara, Wataalam wa Kilimo, wakulima pamoja na viongozi wa Vyama vya Ushirika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB Bw.Asangye Bangu alipongeza uongozi wa Mkoa wa Geita kwa kuuza Choroko msimu wa 2024/2025 kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, na kutoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya WRRB. Alisisitiza kuwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ni mfumo wa wazi, unaohitaji ushirikiano wa kila mdau ili kuleta manufaa yaliyokusudiwa. Aidha, aliwapongeza wakulima kupitia Chama Kikuu cha Ushirika GCU kwa kutekeleza mfumo na kuwasihi kufanya maandalizi ya mapema hususan upatikanaji wa vifungashio na watoa huduma kuelekea msimu wa 2025/2026.
Vilevile, viongozi waliohudhuria mkutano huo waliipongeza WRRB kwa jitihada zinazoendelea za kusimamia na kueneza Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika maeneo mbalimbali nchini. In english
