Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
WAZIRI AZINDUA MFUMO WA CCTV KAMERA PAMOJA NA STIKA YA UTAMBUZI WA GHALA
01 Feb, 2025
WAZIRI AZINDUA MFUMO WA CCTV KAMERA PAMOJA NA STIKA YA UTAMBUZI WA GHALA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo  tarehe 31 Januari 2025 Jijini Dodoma amezindua mfumo wa cctv kamera pamoja na stika ya utambuzi wa Ghala, kamera hizo zitazoweza kusaidia kusimamia Ghala nyakati zote za misimu na kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo upotevu wa mazao katika ghala ,

 

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Jafo amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa WRRB Asangye Bangu pamoja na Bodi nzima ya stakabadhi za ghala kwa ubunifu huu unaoenda kusadia wakulima kuepukana na changamoto zinazotokea mara kwa mara katika Ghala.

 

"Kipindi cha nyuma baadhi ya korosho zilichanganywa  mchanga na mawe mpaka soko la Korosho Tanzania likapata mtikisiko sababu ya kutokuwepo uangalizi,

Lakini leo hii mfumo wa kamera  unatupa uhakika wa kuyaona mazao katika ghala tukiwa huku huku makao makuu,tunapata hata ujasiri kwa wanunuzi wanaona wananunua zao likiwa katika ubora" alisema Mhe. Jafo

 

Bodi ya Stakabadhi za Ghala imeanza kwa Hatua ya kwanza kwa kufunga kamera Ghala 13 ambazo zinahifadhi Korosho ,Ufuta na Mbaazi katika Hatua ya pili itayafikia na mazao kama Dengu katika mikoa ya manyara Singida na Tabora