Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
Mhe. Martin Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Geita, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw.Asangye Bangu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala
24 Oct, 2025
Mhe. Martin Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Geita, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw.Asangye Bangu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

Leo tarehe 24 Oktoba 2025, Mhe. Martin Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Geita, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw.Asangye Bangu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, ofisini kwake Geita. Katika majadiliano hayo, Mhe. Shigela ameishukuru Bodi pamoja na wadau wengine ambao ni TCDC, COPRA na TMX kwa kuusimamia mfumo wa stakabadhi za ghala katika Mkoa wa Geita ambapo, mazao ya Dengu na Choroko kwa sasa ndio yanauzwa kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala.
Aidha, ameelekeza watalaam wa Kilimo pamoja na Biashara kuandaa kikao cha wadau wa mfumo wa stakabadhi za ghala kwa lengo la kujiandaa na upatikanaji wa Mbegu bora, pembejeo, Mbolea, na Upatikanaji wa masoko kwa ajili ya msimu ujao wa 2026/2027. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Mwezi Novemba mwaka huu. Pichani Mhe. Shigela pamoja na Bw. Bangu.