Ujumbe wa maafisa kutoka Shirika la Kimataifa mwanachama wa Benki ya Dunia la International Finance Corporation (IFC)
05 Mar, 2023
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu amepokea ujumbe wa maafisa kutoka Shirika la Kimataifa mwanachama wa Benki ya Dunia la International Finance Corporation (IFC), linaloshughulika na kuboresha hali ya kiuchumi kwa wananchi wa nchi zinazoendelea. Aidha, wajumbe kwa pamoja walijadili namna kuimarisha mifumo ya masoko ya mazao na njia bora za uhifadhi ili kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa. Vilevile, kupitia kikao hicho taasisi hizi zimeweka mpango endelevu wa mashirikiano ya kiutendaji baina ya taasisi hizi